Katika dunia hii kuna matajiri pia kuna maskini....Zipo sababu nyingi zinazotofautisha kati ya tajiri na maskini nazo ni kama zifuatazo:
1a.WATU MATAJIRI HUTAFUTA MAFANIKIO.
Watu ambao ni matajiri huelewa ya kuwa katika maisha kila linalotokea hutokea kwa sababu fulani.
Zaidi ya kuamini katika hilo,hufanya kitendo cha haraka katika kupigania ndoto zao kuwa kweli.
Pia huweka pembeni visingizio na kufanya kila linalotakiwa kufanyika.
1b.MASKINI HUTAFUTA MAKOSA.
Watu ambao ni maskini sikuzote huangalia matatizo baadala ya ya suluhisho.Mwisho wa siku huishia kulaumu mazingira yao,hali zao,kazi zao,serikali n.k na wanakuwa na visingizio vingi vya kwanini hawawezi kufanikiwa.
2a. MATAJIRI HUTAMBUA KUWA MUDA NI MUHIMU KULIKO PESA.
Watu matajiri hawajawahi kufanya biashara ya kubadilishana muda kwa hela.
2b. WATU MASKINI HUDHANI PESA NI MUHIMU SANA KULIKO MUDA.
Mamilioni ya watu dunia nzima hufanya kuuza muda wao. Inaweza ukawa unapata 50,000 ila huwezi kuyapata masaa 72 Tena. Asilimia kubwa ya watu wanauuza muda wao kwa kushindwa kutambua uwezo wao.


Fact
ReplyDeletePost a Comment